Uko hapa: NyumbaniHabariDini2021 06 11Article 542185

Habari za Mikoani of Friday, 11 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

NMB Kusini wakabidhi shule 4 samani za Sh mil 20  na meza

NMB Kusini wakabidhi shule 4 samani za Sh mil 20   na meza NMB Kusini wakabidhi shule 4 samani za Sh mil 20  na meza

BENKI ya NMB Kanda ya Kusini imekabidhi samani za shule za sekondari na msingi zenye jumla ya Sh milioni 20 kwa shule za wilaya ya Nachingwea na Lindi mkoani Lindi.

Samani hizo ambazo ni viti, meza na madawati zilikabidhiwa kwa shule za sekondari za Nyengedi iliyopo Lindi ; Sekondari ya wasichana ya Nachingwea, Sekondari ya Ndangalimbo na Shule ya Msingi Mapinduzi zote zipo wilayani Nachingwea.

Akikabidhi viti na meza hizo kwa nyakati tofauti Meneja wa NMB kanda ya Kusini, Janeth Shango alisema benki hiyo inawiwa na watanzania katika kusaidia kuendeleza sekta ya elimu.

Akiwa katika Shule ya Sekondari Nyengedi mkoani Lindi, alisema viti na meza hizo zenye thamani ya Sh milioni tano vimelenga kuchochea maendeleo ya elimu mkoani Lindi pamoja na Halmashauri ya Mtama.

Akipokea madawati ya Shule ya Sekondari Nyengedi, Mkuu wa wilaya wa Lindi Shaibu Ndemanga alisema kwamba msaada huo umefika kwa wakati mwafaka kwani wilaya inapambana kuhakikisha watoto wote wanakaa katika viti.

Naye Mkuu wa Shule ya Nyegendi, Nuru Nabahani alisema pamoja na msaada huo wa viti pia wanahitaji msaada katika ujenzi wa madarasa, vifaa vya maabara na maabara.

Wakati huo huo benki hiyo imetoa jumla ya meza 100 na viti 50 kwa shule tatu, mbili zikiwa ni shule za sekondari wilayani Nachingwea.

Shule zilizonufaika na msaada huo ni Sekondari ya Wasichana ya Nachingwea, Sekondari ya Ndangalimbo na Shule ya Msingi Mapinduzi.

Akikabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika Sekondari ya Ndangalimbo, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango alisema kwamba msaada huo wenye thamani ya Sh milioni 15 ni sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.

Shango alisisitiza Benki ya NMB imeamua kushirikiana na jamii kwa kutoa msaada katika shule hizo tatu, ambapo Shule ya Msingi ya Mapinduzi ilipata madawati 50 huku sekondari zote mbili zikipata viti na meza 50 kila mmoja, ili kusaidia kuwa na taifa linalojitambua .

Akizungumza katika hafla, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba alisema msaada huo ni tunu kwa wananchi wa Nachingwea na Lindi.

Benki ya NMB yenye matawi 225 nchi nzima,mashine za kutolea fedha ATM zaidi ya 800,wakala zaidi ya 6,000 na idadi ya wateja zaidi ya milioni tatu ndio benki bora nchini kwa miaka minane sasa

Join our Newsletter