Uko hapa: NyumbaniHabariDini2021 06 10Article 542023

Habari za Mikoani of Thursday, 10 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

RC Rukwa aagiza marejesho ya mikopo ya Sh mil 316

RC Rukwa aagiza marejesho ya mikopo ya Sh mil 316 RC Rukwa aagiza marejesho ya mikopo ya Sh mil 316

MKUU wa Mkoa wa Rukwa,Joseph Mkirikiti amemwagiza Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga, Jacob Mtalitinya kuwakabili wadaiwa sugu wa mikopo ya halmashauri ifikayo Sh milioni 316/- ifikapo mwisho wa mwezi huu.

Wadau hao sugu ni vikundi vya wanawake,vijana na watu wanaoishi na ulemavu

ambao walikopeshwa na manispaa hiyo mikopo isiyo na riba yenye thamani ya Sh milioni 316/- katika mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni asilimia kumi ya makusanyo ya ndani.

Mkirikiti alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha baraza la madiwani Manispaa ya Sumbawanga kilichojadili hoja za Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2019/20.

“ Hii ni mara yangu ya

kwanza kuhudhuria kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Sumbawanga lakini ninazo taarifa kuwa zaidi ya Sh milioni 316/- zilizokopeshwa na manispaa kama mikopo isiyo na riba kwa vikundi maalumu vya wajasiriamali lakini wameshindwa kuirejesha.

“Hoja yangu hapa ni je! Manispaa ilikopesha vikundi sahihi au iliwapatia watu fedha halafu ikazichukua na kuzitumia ?

“Je! vigezo vilitumika ka-

tika kutoa mikopo hiyo yaani ilitolewa kwa utaratibu upi na Je! upo mfumo madhubuti wa ufuatiliaji? Nitafuatilia kwa karibu hata kama mikopo hiyo itarejeshwa ili ukweli ujulikane” alisisitiza.

Aidha aliwataka madiwani katika kata zao wafuatilie kama kuna wadaiwa hao sugu na kuwa watumie nguvu zao za ushawishi kupitia vikao vya maendeleo ya Kata (WDC) ili mikopo hiyo irejeshwe kabla ya Juni,30 mwaka huu.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa,David Kilonzo aliwataka watendaji wasiwe sehemu ya kusababisha hoja za ukaguzi kwa sababu wanaitwisha manispaa mzigo mzito na kushindwa kutoa huduma ipasavyo .

Awali Kaimu Mweka Hazina Manispaa ya Sumbawanga,Dorothy alieleza sababu Manispaa hiyo kupata hati safi ya ukaguzi mfululizo kwa miaka minne ya fedha kuanzia 2016/2017 hadi 2019/2020.

Join our Newsletter