Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 09 14Article 557422

Habari za Mikoani of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Taarifa kutoka Shinyanga kijana alieruka fensi baada ya kufanya mauaji

Polisi Polisi

Mkazi wa Mtaa wa Nyahanga Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Steven Felician Samandari (25) ambae alikua Mlinzi wa Kampuni ya Mast Holding ameuwawa kwa kuchomwa kisu tumboni na Mtu ambae bado jina lake halijafahamika ambae aliruka fensi kwenye Guest House na Bar aliyokua akilinda Steven.

Mtuhumiwa huyo anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kwa kisu Mlinzi huyo aliyekua akimzuia kuingia eneo hilo usiku kumfuata Mpenzi wake ambae ni Muhudumu wa Guest House hiyo.

Kamanda wa Polisi Shinyanga George Kyando amesema Guest House hiyo ambayo ina Bar hapohapo ilikua imeshafungwa usiku huo na Mtuhumiwa alipofika kutaka kuingia aliambiwa arudi kesho yake kwani muda wa kazi umeshaisha ila hakukubalianana hilo.

“Kilichofata ni yeye kuruka fensi na kuingia, Mlinzi alipomuona akamkamata ili kumtoa nje lakini kumbe alikua na kisu, akamchoma Mlinzi huyo ambae alifia palepale kutokana na kutokwa na damu nyingi, Mtuhumiwa amekimbia lakini tunamshikilia Muhudumu na hadi sasa amegoma kumtaja Mtuhumiwa” ——— RPC Kyando.