Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 09 13Article 557239

Habari za Mikoani of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Umbali wa zahanati wasababisha waogope kubeba mimba

Umbali wa zahanati wasababisha waogope kubeba mimba Umbali wa zahanati wasababisha waogope kubeba mimba

Wanawake wa Kijiji cha Kadashi wilayani Kwimba mkoani Mwanza wamekuwa na wasiwasi kubeba ujauzito kwa kuhofia kutembea umbali wa kilometa 50 kwenda kuhudhuria kliniki kila mwezi hiyo ikitokana na kutokukamilika kwa ujenzi wa kituo cha afya ulioanza miaka tisa iliyopita.

Restuta Balele ni mkazi wa kata ya Maligisu wilayani Kwimba amesema kwa zaidi ya miaka tisa wamekuwa wakihangaika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa 50 kutafuta huduma za afya huku kina mama wakijawa na hofu ya kubeba ujauzito.

Amesema ujenzi wa hospitali ya kadashi umechukua muda mrefu na kuwapa wasiwasi pindi tunapoumwa na kubeba ujauzito tunashindwa kwenda hospitali kuhudhuria kliniki, kupatiwa elimu ya afya hasa ya uzazi mwisho wa siku wanaishia kuzaa bila kupata usaidizi ama ushauri kwa wataalamu wa afya .

Kwa upande wake Patrick Gervas ambae ni mkazi wa kijiji cha Kadashi amesema wagonjwa wengi hupoteza maisha wakiwa njiani kuelekea hospitali ambako ni mbali huku ujenzi wa hospitali hiyo ulioanza tangu mwaka 2012 ukishindwa kukamilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo amesema mfumo wa manunuzi wa uliotumika katika ujenzi wa kituo hicho unapaswa kurekebishwa kwakuwa unatoa mwanya wa kufanyika kwa ubadhirifu huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akiwaonya watendaji waliohusika kukwamisha mradi huo na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria.