Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 09 14Article 557329

Habari za Mikoani of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: Habarileo

Vijana wanne wafa mgodini Butiama

Mgodini Mgodini

Watu wanne wakazi wa mkoa wa Mara wamekufa kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Buhemba wilayani Butiama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longnus Tibishubwamu jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Septemba 9, mwaka huu saa 10:00 jioni kwenye shimo namba sita katika mgodi huo.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mwita (20), Lucas Joseph (21) wakazi wa Tarime, Baraka Christopher (23) mkazi wa Rorya na Enock Filbert (23) mkazi wa kijiji cha Mwitongo wilayani Butiama. Amesema waliokufa ni wachimbaji wadogo katika shimo hilo ambalo awali wataalamu wa madini walilifunga kutokana na kasoro kwenye miundombinu.

“Siku hiyo wataalamu walikwenda kukagua hilo duara wakaridhika na maboresho yaliyofanywa hivyo wakalifungua, sasa wale wafanyakazi walipokuwa wakiingia duarani kamba waliyokuwa wakitumia kushuka ikakatika wakaangukia ndani na kufariki papo hapo,” amesema Kamanda Tibishubwamu.