Uko hapa: NyumbaniHabariMikoani2021 09 06Article 555424

Habari za Mikoani of Monday, 6 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watumishi 15 wafukuzwa kazi Uyui

Watumishi 15 wafukuzwa kazi Uyui Watumishi 15 wafukuzwa kazi Uyui

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora limewafukuza kazi watumishi 15. Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi alisema hayo jana wakati wa kikao cha robo ya nne cha baraza hilo.

Ntahondi alisema watumishi hao walifukuzwa kwa sababu ya makosa ya utoro kazini na wengine walikutwa na vyeti vya bandia (vyeti feki). Alisema watuhumiwa 28 waliokuwa waliokabiliwa na tuhuma mbalimbali wamefutiwa makosa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kuwatia hatiani.

Ntahondi alisema Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Halmashauri hiyo imemwondoa Mtendaji wa Kata ya Nsololo na kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji ampeleke Mtendaji mwingine baada ya kubaini aliyekuwepo alishindwa kumudu majukumu.

Alisema pia wamemsimamisha Fundi Sanifu wa Halmashauri hiyo kupisha uchunguzi baada ya kubainika mapungufu katika ujenzi wa baadhi ya maabara wilayani humo. Ntahondi aliwaagiza wakuu wa idara katika halmashauri hiyo wawasimamie watumishi chini yao ili watoe huduma bora kwa wananchi.