Uko hapa: NyumbaniDini2019 11 14Article 487612

Dini of Thursday, 14 November 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

Askofu Shoo ataka haki uchaguzi serikali za mitaa

Askofu Shoo ataka haki uchaguzi serikali za mitaa

Dar es Salaam. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amesema mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa usipotendeka kwa haki unaweza kusababisha fujo.

Kauli ya Shoo imekuja wakati serikali ikitangaza kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa huku  wapinzani wakitangaza kujiondoa kwa kile wanachodai kutotendewa haki.

Askofu Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini amesema kuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo anayo dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani sawa.

“Msimamizi mkuu wa uchaguzi anayo dhamana kubwa ya kuhakikisha kunakuwa na `fair play’ (usawa) kwa vyama vyote bila upendeleo.”

“Zoezi hili lisipofanyika kwa haki linaweza kusababisha fujo na uvunjifu wa amani. Wito wangu kwake na wasimamizi wengine wote wasimamie haki,” alisema Askofu Shoo.Join our Newsletter