Uko hapa: NyumbaniDini2019 11 14Article 487597

Dini of Thursday, 14 November 2019

Chanzo: mwananchi.co.tz

Askofu asikitishwa wapinzani kujitoa, aomba uchaguzi uahirishwe

Askofu asikitishwa wapinzani kujitoa, aomba uchaguzi uahirishwe

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Owdenburg Mdegela amesema ni vizuri kwa wanasiasa kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kupata suluhisho linaloweza kusaidia vyama hivyo kuingia kwenye chaguzi.

Askofu Mdegela ametoa maoni hayo ikiwa ni siku kadhaa baada ya vyama kadhaa vya upinzani vikiwemo Chadema na ACT- Wazalendo kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa madai ya kutokuridhika na mchakato huo.

“Kwa nini wasiahirishe uchaguzi kwanza ili mambo ya siasa yakae sawa? Kujiondoa kwa upinzani mimi nimehuzunika, sikufurahia kabisa kwa sababu tunahitaji upinzani ili mambo yakae sawa.

“Kwa kazi nzuri aliyoifanya Rais Magufuli (John) hili jambo linaweza kuleta doa. Pamoja na ukorofi wa wapinzani bado wanatakiwa kupewa nafasi ya kuingia kwenye uchaguzi,” amesema askofu huyo

Alionya nchi kwa sasa ikikosa upinzani itasababisha matatizo kidogo na ikiendelea hivi mwakani italeta doa kwenye uchaguzi wa rais na wabunge.

SOMA ZAIDI

Join our Newsletter