Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 14Article 563188

Soccer News of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ajibu Aanza Kunoga Simba

Ibrahim Ajib Ibrahim Ajib

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu ameanza kuonesha cheche zake ndani ya kikosi hicho kufuatia jana kutoa asisti murua katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Cambiasso Academy.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Boko, Dar, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, huku bao la Simba likifungwa na Henock Inonga Baka akimaliza pasi ya Ajibu aliyepiga mpira wa faulo.

Simba ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana utakaochezwa Oktoba 17, mwaka huu nchini Botswana kabla ya kurudiana Dar.

Ajibu chini ya Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amekuwa hana nafasi ya kutosha lakini kwenye mchezo huo wa kirafiki alipopewa nafasi, akafanya kweli.

Kabla ya kupiga faulo hiyo, Ajibu aliutenga mpira vizuri, kisha akaupiga kwa ufundi mkubwa na kupatikana kwa bao hilo la kuongoza kabla ya Cambiasso kusawazisha. Ajibu amekuwa fundi wa asisti akikumbukwa msimu wa 2018/19 wakati akiwa Yanga akimaliza Ligi Kuu Bara na asisti 17.