Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556651

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Biashara United yasafiri dakika za lala Salama

Kikosi cha Biashara United kikiwa Uwanja wa ndege tayari kwa Safari Kikosi cha Biashara United kikiwa Uwanja wa ndege tayari kwa Safari

Leo Ijumaa kikosi cha Biashara United kinatarajiwa kushuka dimbani kwenye mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Dakhil FC ya Djibouti katika dimba la Stade du Ville majira ya saa tisa alasiri.

Namna walivyosafiri Timu ya Biashara United ndio ambavyo inatia shaka kwani inaonesha dhahiri hawakujiandaa ama hawajui nini cha kufanya linapokuja suala la michuano ya Kimataifa.

Kikosi hicho kilipanga awali kuondoka siku ya Jumatano Septemba 7 alfajiri kwa kupitia Ethiopia lakini ilishindikana kusafiri kwa sababu ambazo zimesemekana kuwa ni kitendo cha nyota wake kukosa hati za kusafiria.

Baadae uongozi wa klabu hiyo ulikiri kuwa changamoto haikuwa hati za kusafiria bali ni masuala ya Viza, na hivyo wataondoka Alhamis alasiri lakini bahati mbaya mpaka jana majira ya saa tatu usiku timu hiyo bado ilikuwa katika kambi yao maeneo ya Ilala huku wakidai wataondooka usiku huo wa Alhamis.

Biashara United inashiriki michuano hii kwa mara ya kwanza tangu ipande daraja msimu wa 2018/19 na hii ni baada ya timu hiyo kumaliza kwenye nafasi nne za juu msimu uliopita.

Sasa Alfajiri ya Leo Biashara wamesafiri kuelekea Nchini Djibout na wameshashuka Ethiopia kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea Djibouti.

Biashara United wanaingia katika mchezo huo pasipo kusoma mazingira ya eneo wanalokwenda kucheza mechi, wanaingia katika mchezo huo pasipo kufanya mazoezi yanayoridhisha ya dakika za mwisho.

Kuna kila dalili za Biashara kufanya vibaya katika mchezo huo japokuwa Mwalimu wa kikiosi hicho amewataka mashabiki na watanzania waondoe hofu kwani wamejipanga vya kutosha.