Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585895

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Breaking: Chama Awasili Tanzania Kujiunga na Simba Sc

Chama Akiwasili Chama Akiwasili

HATIMAYE aliyewahi kuwa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Clatous Chota Chama, amewasili nchini jioni hii ya leo Januari 14, 2022 kujiunga tena na mabingwa hao wapywa wa Mapinduzi Cup na Mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi Kuu.

Chama ambaye ni raia wa Zambia amejiunga na Simba akitokea Rs Berkane ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili na amewakili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwao Zambia.

Alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuondoka mwaka 2021 kabla ya kurejea Simba na kutambulishwa rasmi leo ambapo bango kubwa lililotolewa na Simba likiwa na picha ya Chama linasomeka “Karibu nyumbani, Welcome home.”

Chama aliondoka Simba Augusti 13,  2021 na kujiunga  na RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco.

Berkane imesema sababu kubwa ya Chama kuondoka Morocco ni kushindwa kuzoea mazingira ya nchi hiyo kwa haraka pamoja na masuala ya kifamilia.