Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556678

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

CAF yapiga kimya sakata la nyota wa Yanga

Nyota wa Yanga waliozuiliwa kushiriki Ligi ya Mabingwa na CAF Nyota wa Yanga waliozuiliwa kushiriki Ligi ya Mabingwa na CAF

Klabu ya Yanga Septemba 12, siku ya Jumapili itatupa karata yake ya kwanza katika Michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika msimu huu dhidi ya Rivers United kutoka nchini Nigeria.

Kiungo Khalid Aucho, Straika Fiston Mayele na beki Djuma Shaban wamezuiliwa na CAF baada ya kukosa hati za uhamisho wa Kimataifa kwa maana ITC zao hazijawafikia CAF.

Katika Mkutano wao na waandishi wa Habari kati kati ya wiki hii, Yanga wamesema kupitia TFF wameshaliandikia Shirikisho la Mpira Afica (CAF) barua ya kujieleza na kuwaomba iwaruhusu wachezaji hao.

Huku zikiwa zimebaki siku mbili kushuka katika mtanange huo, bado hakuna taarifa yoyote inayoonesha kama wachezaji hao watatu wa kimataifa ya Yanga wanaweza kuwa ni sehemu ya kikosi siku ya Jumapili.

Akithibitisha hilo msemaji wa Yanga haji Manara amesema bado hawajapata taarifa yoyote kutoka CAF linalohusiana na sakata la wachezaji hao, ila wanatumai mechi ya mkondo wa pili watajiunga na kuwa sehemu ya kikosi.