Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 25Article 574027

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

CEO Bodi ya Ligi azungumzia utata wa Penati ya Yanga

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), Almasi Kasongo amesema mpaka sasa makosa ya waamuzi yaliyojitokea katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ni ya kibinadamu kuliko watu wanavyofikiria.

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22 inaelekea mzunguuko wa saba, huku Wadau wengi wa Soka wakilalamika kuhusu maamuzi ya baadhi ya waamuzi waliochezesha michezo ya mizunguuko sita iliyopita.

Kasongo ametoa kauli hiyo, kufuatia malalamiko yanayoelekezwa kwa mwamuzi Abel William wa Arusha aliyechezesha mchezo kati ya Namungo FC na Young Africans uliounguruma Jumamosi (Novemba 20) na kumalizika kwa sare ya 1-1, Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.

Mwamuzi Abel William aliibua sintofahamu kupitia maamuzi yake ya Mkwaju wa Penati, ulioiwezesha Young Africans kupata bao la kusawazisha.

Kasongo amesema TPBL imekua ikifuatlia kila mchezo na kujiridhisha Mazuri na Mapungufu yaliyojitokeza, na wamebaini mpaka sasa yaliyojitokeza na kulalamikia yaliyokua ni ya kibinadamu kuliko watu wanavyofikiria.

“Kwa utaratibu wetu kila mchezo unapomalizika tunakaa kikao kupitia matukio mbalimbali, hivyo ni suala la kamati kutoka na majibu kwa kile walichokibaini,” amesema Kasongo.