Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 23Article 573607

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Carrick hajali muda atakaodumu United

Michael Carrick, Kocha wa Muda Man United Michael Carrick, Kocha wa Muda Man United

Kocha wa Muda wa Manchester United, Michael Carrick, amesema jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ndilo kubwa na sio kuzingatia atadumu kwa muda gani ndani ya nafasi hiyo.

Carrick kwa sasa ndio kocha wa muda wa Man United, baada ya kuondoka kwa Ole Gunnae Solskjaer.

"Nimejiandaa kufanya kazi hii kwa mud wowote nitakaokuwa hapa, iwe ni mchezo mmoja, michezo miwili japokuwa kwa sasa sina uhakika ila sifikirii masuala ya muda kwa sasa, nawaza ya kesho" amesema Carrick

Manchester United kwa sasa inakabiliwa na mchezo wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Villareal ugenini, na huo ndio utakua mtihani wa kwanza kwa Michael Carrick.