Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585727

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Chama atambulishwa Msimbazi, Shughuli zimesimama

Clatous Chotta Chama Clatous Chotta Chama

Hatimaye kile kizungumkuti cha anakwenda wapi? aidha Simba au Yanga? kimepata jibu baada ya Kiungo wa Kimataifa wa Zambia Clatous Chotta Chama kutambulishwa katika viunga vya Msimbazi.

Simba wanamrudisha Chama ikiwa ni miezi michache tu tangu aondoke kwenda kujiunga na RS Berkane ya nchini Morocco.

Chama alijiunga na Simba mwaka 2018 na kuondoka mwaka 2021 kabla ya kurejea tena Simba.

Chama aliondoka Simba SC August 13 2021 na kujiunga na Club ya RS Berkane ya Morocco na sasa anarejea baada ya kudaiwa kushindwa kuzoea mazingira nchini Morocco, masuala ya kifamilia nk

Tazama taarifa ya utambulisho wake ndani ya Simba SC.