Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585745

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ebwana eeh, Kumbe Yanga hawajatoka kizembe Mapinduzi Cup

Ibrahim Bacca Ibrahim Bacca

Kama ulidhani Yanga imetoka kizembe tu katika Michuano ya Mapinduzi Cup kule visiwani Zanzibar unajidanganya.

Kweli Yanga walitoka hatua ya nusu fainali ya Michuano ya Mapinduzi Cup lakini wamerudi na mtaji, kutokea Zanzibar.

Yanga wamemsajili Mlinzi Ibrahim Bacca kutokea KMKM ya visiwani Zanzibar, klabu ambayo katika michuano ya Mapinduzi ilikipiga na Yanga wakatoa sare ya magoli 2-2.

Ibrahim Bacca anacheza kama mlinzi wa kati lakini pia ana uwezo wa kukipiga kama full beki wa pembeni.

Pengine hiyo inaweza kuwa ahueni kwa Mabingwa hao mara 27 wa Tanzania kwa kuwa hivi sasa wanamkosa Kibwana Shomari na Djuma Shabani katika maeneo ya walinzi wa pembeni.