Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 13Article 585481

Soccer News of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fainali Mapinduzi Cup: Mashabiki Wafurika Zenji

Fainali Mapinduzi Cup: Mashabiki Wafurika Zenji Fainali Mapinduzi Cup: Mashabiki Wafurika Zenji

Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar wamejitokeza kwa wingi mapema asubuhi kuwahi tiketi kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Azam.

Mchezo huo ambao mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Utapigwa leo saa Moja jioni katika Uwanja wa Amaan.

Fainali hiyo inakutanisha miamba ya soka katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara huku timu zote zikitambiana kutwaa taji hilo kutokana na ubora wa timu zote katika kutandaza soka la kuvutia na la kiufundi.

Simba ilitinga fainali kwa kuisukuma nje ya michuano hiyo Namungo FC kwa mabao 2 -0, huku Azam ikiwatupa nje mabingwa watetezi Yanga kwa mikwaju ya penalti 9-8.