Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 09Article 562336

Soccer News of Saturday, 9 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Fei toto aweka rekodi Yanga

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum katika mechi dhidi ya Geita Gold Kiungo wa Yanga, Feisal Salum katika mechi dhidi ya Geita Gold

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameweka rekodi ndani ya Yanga mara baada ya kufanikiwa kuiongoza timu hiyo kushinda michezo miwili mfululizo ya ligi kuu akiwa na kitambaa cha unahodha wa kikosi hicho.

Tangu ajiunge na Yanga mwaka 2018, Fei Toto hakuwahi kuwa nahodha wa Yanga katika mechi za kimashindano walizocheza.

Msimu huu wakati nahodha mkuu Bakari Mwamnyeto akiwa majeruhi, Fei Toto amekiongoza kikosi hicho katika michezo dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold ambayo yote Yanga imeshinda kwa bao 1-0, huku Fei Toto akifunga bao moja la ushindi dhidi ya Kagera Sugar.

Fei Toto alisema anafurahia kuona amefanikiwa kuiongoza Yanga kushinda michezo hiyo akiwa ni nahodha, huku akiweka wazi kuwa bila nguvu ya wachezaji wengine hilo lisingekamilika.

“Nashukuru kwa kuwa ni jambo jema, sikuwahi kufikiria hili lakini kwa kuwa limetokea tumeshinda michezo yote miwili nikiwa kama nahodha, nashukuru sana.

“Hii ni maana halisi ya kuwa na ushirikiano kwani peke yangu nisingeweza kufanikisha ushindi tulioupata, tulishirikiana vema wachezaji, waalimu na mashabiki waliojitokeza kutupa hamasa ya kushinda, tukafanikiwa,” amesema Fei Toto.