Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 22Article 573595

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Gareth Southgate asaini Mkataba mpya England

Gareth Southgate Gareth Southgate

Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi, kocha wa Timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate, ameongeza mkataba mpaka 2024.

Southgate alikuwa akiutumikia mkataba wa kuiongoza timu hiyo ambao ungefikia tamati siku za usoni. Kufuatia hatua chanya zinazopigwa na timu hiyo, ni dhahiri Southgate anastahili mkataba mpya.

Gareth Southgate ameiongoza Uingereza kwenye fainali ya Euro 2020 bila kupoteza mchezo wowote (ukiacha fainali) na ameendelea kufanya vizuri zaidi baada ya kuivusha timu hiyo na sasa, Uingereza ni miongoni mwa timu za awali kufuzu Kombe la Dunia, 2022.

Huu ni muendelezo wa Southgate kuendelea kukinoa kikosi cha Timu ya Taifa ambapo alianza kazi hiyo mwaka 2016.