Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556627

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Gomes nje mechi za Simba klabu bingwa

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF, limetoa orodha ya Makocha ambao hawaruhusuwi kukaa kwenye benchi la timu zao, kutokana na kukosa vigezo vya CAF A au UEFA PRO LICENCE.

Katika Orodha hiyo yumo kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes ambae hajakidhi vigezo hivyo ambapo yeye ana (UEFA A Diploma).

Katika orodha hiyo yumo pia kocha Ame Khamis, wa KMKM ya visiwani Zanzibar ambae nae timu yake inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gomes aliifikisha Simba SC hatua ya robo fainali msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini.