Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 14Article 557344

Soccer News of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Horseed kukipiga Chamazi kama wenyeji

Kikosi cha Horseed FC, kitaikabili Azam Septemba 18 Kikosi cha Horseed FC, kitaikabili Azam Septemba 18

Mchezo wa Mkondo wa Pili wa marudiano Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Horseed FC kutroka nchini Somalia na wawakilishi wa Tanzania, Azam FC utapigwa Jumamosi ya Septemba 18 katika dimba la Azam Complex na si Uwanja wa Uhuru kama ilivyotangazwa awali.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Azam, Thabit Zakaria "zaka zakazi" amesema Horseed FC wameamua kuomba mchezo huo kurudishwa Chamazi kutokana na ubora wa Uwanja huo katika suala zima la miundombinu iliyopo kwa Matajiri hao wa Jiji.

“Horseed wameamua kuamisha mechi yetu Azam Complex baada ya mechi yetu ya awali kupangwa kuchezwa Uhuru na sababu kubwa ni wao kuridhishwa na miundombinu iliyopo Chamazi” anasema Zakaria

Mechi ya kwanza Azam ilishinda mabao 3-1 wakiwa wenyeji wa mechi hiyo, na mechi ya pili watarudi kama wageni.

Hali hiyo imetokana na Usalama kutokuwa wa kuridhisha nchini Somalia.