Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 07 19Article 547417

Soccer News of Monday, 19 July 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

JKT, Ihefu, Gwambina zaungana na Mwadui Ligi daraja la kwanza

JKT, Ihefu, Gwambina zaungana na Mwadui Ligi daraja la kwanza JKT, Ihefu, Gwambina zaungana na Mwadui Ligi daraja la kwanza

Ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar umeshindwa kuinusuru JKT Tanzania katika vita ya kushuka daraja.

Timu hiyo sanjari na Gwambina, Ihefu na Mwadui zimeaga rasmi Ligi Kuu na msimu ujao zitacheza Ligi daraja la kwanza.

JKT Tanzania imeshuka daraja ikiwa na pointi 39 baada ya kuichapa Mtibwa Sugar katika mechi ya mwisho leo.

Ihefu imeporomoka ikiwa na pointi 35 baada ya kuruhusu kipigo cha bao 1-0 dhidi ya KMC.

Gwambina licha ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons, matokeo hayo yameshindwa kuinusuru na dhahama ya kushuka daraja.

Mwadui ambayo ilicheza mechi ya kuhitimisha ratiba baada ya kuporomoka daraja siku nyingi imehitimisha msimu kwa kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

Mechi nyingine, Coastal Union imeichapa mabao 3-1 Kagera Sugar.