Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 21Article 573163

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Jahazi la Mtibwa lazidi kuzama, yachapwa tatu ugenini

Mtibwa Sugar yapoteza ugenini Mtibwa Sugar yapoteza ugenini

Wewnyeji, Timuu ya Mbeya City wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 45, Juma Shemvuni dakika ya 60 na Suleiman Ibrahim dakika ya 85, wakati la Mtibwa limefungwa na Salum Kihimbwa dakika ya 82 kwa penalti.

Kwa ushindi huo, Mbeya City inafikisha pointi 10 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi wastani wa mabao tu Polisi Tanzania baada ya wote kucheza mechi sita, wakati Mtibwa inabaki na pointi zake mbili za mechi sita sasa katika nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.

Mtibwa inazizidi wastani wa mabao tu Geita Gold na KMC zilizo chini yake mkiani kwenye eneo la kushuka moja kwa moja.

Ikumbukwe timu zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.