Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 13Article 557095

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

KMKM yaanza vibaya Kimataifa, Mafunzo yatepeta nyumbani

Mchezaji wa KMKM FC, akimiliki Mpira mbele ya mchezaji Al Ittihad Mchezaji wa KMKM FC, akimiliki Mpira mbele ya mchezaji Al Ittihad

Wawakilishi wa Tanzania Visiwani katika Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya KMKM imeanza vibaya michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa klabu ya Al Ittihad kutoka nchini Libya.

Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Amaan, Zanzibar, hazikuhudhuriwa na mashabiki baada ya Shirikisho la Soka Afrika kuzuia kutokana na mapambano ya janga la Corona.

Mechi hiyo awali ilikuwa ichezwe Septemba 11 lakini ikaaihirishwa na kuchezwa Septemba 12 majira ya saa nane mchana.

Magoli ya Al Ittihad yamefungwa na Muad Eisay dakika ya 45, na Rabia Alshadi dakika ya 84 na kuwapa ushindi wageni hao katika mechi hiyo ya mkondo wa Kwanza hatua za awali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo mwingine wa Kombe la Shirikisho barani Afrika timu kutoka visiwani humo, Mafunzo nayo imepoteza kwa goli 1-0 kutoka kwa Interclube ya nchini Angola, goli ambalo limefungwa na Antonio Justo kipindi cha kwanza 29'.