Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 14Article 557347

Soccer News of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kama si kifo, pengine tungejua kwa nini Hans Poppe alitaka kumpindua Nyerere

Marehemu Zacharia Hans Poppe (wa mbele) Marehemu Zacharia Hans Poppe (wa mbele)

Crescentius Magori, Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Mohamed Dewji amesema, kifo cha Zacharia Hans Pope (64) ni pigo kubwa ndani ya timu hiyo.

Hans Pope alifikwa na mauti tarehe 11 Septemba 2021, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu na mwili wake, umeagwa Jumatatu, 13 Septemba 2021, katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar.

Mwili wa Hans Pope aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Simba na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa mabingwa hao mara nne mfululizo wa Tanzania Bara, utazikwa Septemba 15 2021, kijijini kwao Kihesa Mkimbizi, Mkoa wa Iringa.

Magori ametumia dakika zisizozidi 15 kuelezea jinsi walivyoishi na Hans Pope ndani na nje ya timu hiyo huku akidokeza jinsi alivyomuuliza mkasa wa Hans Pope, akiwa Luteni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na wenzake kutaka kumpindua Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo Hans Pope akiwa na miaka 28.

“Kuna siku tukiwa kwenye stori, nikamuuliza ulifikiria nini ukiwa na miaka 28 tu kutaka kupindua na kumpindua mtu mwenyewe ni Mwalimu Nyerere? Akasema anatamani sana kuandika kitabu lakini wenzangu tuliokuwa nao hawataki waandikwe lakini hao watu wanaokataa kama wakifariki kabla yake basi ataandika kitabu lakini Mungu amemchukua kabla hajaandika” amesema Magori.