Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 25Article 573982

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Kichapo cha City ni somo kwa PSG na Pochettino

Nyota wa PSG wakiwa hawaamini kilichotokea Nyota wa PSG wakiwa hawaamini kilichotokea

Wenyeji, Manchester City wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Paris Saint-Germain katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana ndani ya dimba la Etihad.

Kylian Mbappe alianza kuifungia Paris Saint-Germain dakika ya 50, kabla ya Man City kuzinduka kwa mabao ya Raheem Sterling dakika ya 63 na Gabriel Jesus dakika ya 76 na kwa matokeo hayo zote zinafuzu hatua ya 16 Bora.

Mchezo ulikua na ushindani wa hali ya juu na timu zote zilicheza soka la kuburudisha na la viwango vya hali ya juu.

Man City walicheza kitimu zaidi, walipress kwa pamoja na walirudi nyuma kwa pamoja ( shambulia pamoja , zuia pamoja ) lakini PSG kwenye kuzuia ilikuwa jukumu la wachezaji 7 tu watatu wa mbele wanatembea , wakipata mpira ndio wanakuwa wapo uwanjani . Walitegemea zaidi ubora wao kuliko kujituma , dhidi ya City unahitaji kila mtu ajitume.

Udhaifu wa Neymar Mbappe na Messi kurudi nyuma kuzuia ndio uliwapa City mwanya wa kuwaadhibu na magoli yote yamepatikana kwa City kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji upande mmoja halafu kubadilisha haraka mpira upande mwingine ( create overloads and switching play ) . Pasi ya Rodri kwa Walker na Pasi ya Mahrez kwa Bernardo.

Hivyo kamaPSG na Pochettino wana wazo la kutaka kubeba ubingwa wa Ulaya wanatakiwa kuepuka makosa yote yaliyojibainisha katika mechi yao dhidi ya City.

Manchester City inaongoza Kundi A kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na PSG nane, RB Leipzig nne sawa na Club Brugge.