Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585712

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Liverpool yakomaliwa sare na Arsenal iliyo pungufu

Faulo iliyomsababishia kadi nyekundu kiungo wa Gunners, Granit Xhaka Faulo iliyomsababishia kadi nyekundu kiungo wa Gunners, Granit Xhaka

Licha ya kuwa pungufu kwa zaidi ya dakika 60 Arsenal wamelazimisha sare tasa na Liverpool katika mtanange wa kwanza wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Carabao mchezo uliopigwa dimba la Anfield Leo Alhamis.

Granit Xhaka alionyeshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 24 ya mchezo kufuatia nyota huyo wa kimataifa wa Uswisi kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Liverpool Diogo Jota wakati akijaribu kufunga goli kupitia pasi ya Andrew Robertson.

Licha ya kuwa pungufu Arsenal walijipapatua na kupata shuti lililolenga goli kunako dakika ya 71 ambapo Liverpool pia walijaribu kupitia kwa Takumi Minamino ambaye mpira wake ulipita kidogo juu ya mwamba.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa dimba la Emirates Alhamis ijayo.

Mshindi atakutana na Chelsea katika mchezo wa fainali utakaopigwa mwishoni mwa mwezi wa pili baada ya kushinda goli 3-0 dhidi ya Tottenham.