Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 11Article 584956

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Liverpool yawashika Chelsea Pabaya kwa Kounde

Jules Kounde Jules Kounde

Soko la usajili halina mwenyewe. Yeyote anaweza kuchukuliwa na timu yeyote. Mpango na ushawishi wa vilabu ndio vitu muhimu. Liverpool kuwagusa Chelsea kwenye mshono.

Wakati msimu huu ukiwa unaendelea, kuna ishara za jahazi la The Blues kutoboka ifikapo mwishoni mwa msimu huu. Christensen, Azpilicueta na Rudiger wote wanamaliza mikataba yao mwismu huu. Hakuna yeyote kati yao anayeonekana kusaini mkataba mpya mpaka sasa.

Likitokea la kutokea, huu ni mshono ambao Chelsea wanakazi kubwa ya kuutibu. Kama sio kuanzia dirisha hili la usajili, basi wajipange kikamilifu kwenye dirisha kubwa. Mchongo unaungua pale ambapo, vinaingia vilabu vikubwa na vyenye ushawishi mkubwa kwenye mipango yako.

Liverpool wapo tayari kutengua mkataba wa Jules Kounde kule Sevilla. The Blues walidemadema kwa miezi 3 wakihusishwa na Kounde lakini, hawakumsajili. Real Madrid nao ni vivyo hivyo. Kumbe The Reds walikua wanaangalia mambo yanavyokwenda.

Sasa, Jurgen Klopp yupo tayari kulipa Pauni milioni 75 ili kumsajili Kounde kwenye dirisha hili la majira ya baridi. Licha ya kuwa na idadi kubwa ya mabeki kwenye kikosi chao, bado Liverpool wanamuona Kounde kama ni fursa ambayo wanapaswa kuitumia mapema mwezi huu kabla ya msimu kumalizika.

Wakati Chelsea wakiendelea kushangaa shangaa, huenda wakaambulia kupigwa na kitu kizito kwa Kounde kwenda Anfield huku Rudiger akitimkia Santiago Bernabeu mwishoni mwa msimu huu.