Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 22Article 573592

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Lukaku kuwakosa Juventus Darajani

Lukaku hati hati kuikosa Juve Lukaku hati hati kuikosa Juve

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne kocha Thoams Tuchel hana uhakika kama Romelu Lukaku anaweza kurejea kwa ajili ya mchezo huo wakati pia Kai Havertz hatocheza kabisa.

Chelsea watawakaribisha timu ya Juventus katika uwanja wa Stamford Bridge kwaajili ya mchezo wa marudiano kwenye Champions League.

Lukaku amekuwa nje ya dimba yapata mwezi sasa sababu ya jeraha la kifundo cha mguu lakini ni kama yupo karibu kupona kabisa.

Starika huyo alikuwa ameanza mazoezi na timu ya Chelsea wiki iliyopita lakini Tuchel hana haraka ya kumchezesha kwenye mchezo wa Jumanne.

“Sina uhakika bado. Alionekana yuko sawa mazoezini jana Jumapili, tutaangalia kuhusu majibu.

“Ana miadi na madaktari. Labda tunaweza kuweka wachezaji 20 kwenye kikosi. Dakika za mwisho zingekuwa za juu kabisa.

“Jorginho yuko sawa kabisa. Kai alikuwa na tatizo la misuli ya paja hivyo tulimtoa na tuna mashaka naye.