Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 11Article 562540

Soccer News of Monday, 11 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Madagascar yaisafishia njia Stars Kombe la Dunia 2022.

Mtanange wa Stars na Benin Mtanange wa Stars na Benin

Ndivyo ilivyo, baada ya timu ya Tanzania, Taifa Stars kuibuka na ushindi wa goli 1-0 ikiwa ugenini katika mechi ya mapema dhidi ya Benin ndani dimba la Mahamasina, majira ya saa 4:00 usiku kulikuwa na mechi nyingine ya kundi J, kati ya Madagascar dhidi ya DR. Congo.

Madagascar ndio timu pekee ambayo kabla ya mchezo wa jana Oktoba 10 haikuwahi kushinda mchezo wowote katika kundi hilo na ilipoteza michezo yote mitatu.

DR Congo waliokuwa wananyemelea uongozi wa kundi walijikuta wakipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Madagascar na kupoteza matumaini ya kukaa kileleni mwa kundi hilo.

Kazi imekua rahisi kwa Taifa Stars kwani yeye ndio kinara katika kundi na amebakiza mechi mbili tu, dhidi ya madagascar ugenini na DR Congo kwa Mkapa Jijini Dar es Salaam ili kukamilisha hatua hii ya makundi.

Msimamo wa Kundi J, kwa sasa ulivyo kinara ni Taifa Stars akiwa na alama 7 akishuka dimbani michezo minne, nafasi ya pili inakamatwa na Benin akiwa na alama 7, nafasi ya tatu DR. Congo akiwa na alama tano na anaeburuza mkia ni Madagascar akiwa na alama 3.