Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 23Article 573781

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Man United yashinda ugenini, Carrick akianza na ushindi

Wachezaji wa Man United wakishangilia goli la Ronaldo Wachezaji wa Man United wakishangilia goli la Ronaldo

Kikosi cha Manchester United kimetengeneza mazingira ya kutinga hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Villareal ugenini.

Katika mchezo huo uliokuwa wa kwanza kwa Kocha wa muda wa Mashetani wekundu, Michael Carrick ulishuhudia mabadiliko makubwa mawili ikiwemo kuanza kwa Kiungo wa Kidachi Donny Van de Beek na Jadon Sancho.

Magoli ya Man United katika mchezo huo yamefungwa na Cristiano Ronaldo dakika ya 78 ya mchezo na Jadon Sancho ambae amefunga goli kwa mara ya kwanza tangu asajiliwe United dirisha lililopita.

David de gea alifanya kazi kubwa katika mchezo huo kuhakikisha United wanaondoka na alama tatu, baada ya kuokoa mashambulizi kadhaa ya hatari langoni mwa United.