Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 25Article 573991

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mashabiki elfu 35000 kuishangilia Simba kwa Mkapa

Mashabiki 35000 wataishuhudia Simba ikikipiga dhidi ya Red Arrows Mashabiki 35000 wataishuhudia Simba ikikipiga dhidi ya Red Arrows

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu mashabiki 35,000 kuingia uwanjani kushuhudia mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Uongozi wa klabu umepokea barua rasmi kutoka CAF ikiwa na maelekezo hayo ambayo tunapaswa kuyafuata.

CAF imekuwa na utaratibu wa kuruhusu idadi fulani ya mashabiki kuingia uwanjani kwa ajili ya kujikinga na janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Pamoja na mambo mengine, CAF imesisitiza kufuatwa kwa taratibu zote za kujikinga na ugonjwa huo kama kukaa kwa nafasi baina ya mtu na mtu na kuvaa barakoa kwa kila atakayehudhuria.

Tayari viingilio vya mchezo ambapo Mzunguko Sh 5,000, VIP B na C Sh 20,000 na VIP A Sh 40,000.