Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 13Article 557155

Soccer News of Monday, 13 September 2021

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Masikitiko ya Dalali kwa Hans Poppe ni haya

Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali

Aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali amesema kinachomuumiza zaidi ni Zacharia Hans Poppe kuikosa "Simba Day" Jumapili kutokana na namna alivyokuwa amejipanga.

Hans Poppe amefariki dunia Ijumaa Septemba 10 akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam.

Dalali ameiambia amesema kuwa, kifo cha Poppe ni pigo kubwa kwa Simba na tasnia ya mpira wa miguu kwa ujumla.

Amesema namna Hans Poppe alivyokuwa akijitokea katika kila kitu mpaka Simba Day hakutaka kukosa na alikuwa akisapoti kwa asilimia 100 ifanyike kwa ufanisi.

"Nimeumia sana msiba huu mzito anaenda kuikosa Simba Day tamasha ambalo alikuwa akilipenda vilivyo na kulipigania lifanyike kwa ufanisi mkubwa,"

Dalali amesema licha ya shughuli zake nyingi kuwa Mkoani kwa sasa lakini msiba huu umemkuta akiwa Dar es Salaam hivyo ameweza kujumuika na wenzake kumsindikiza marehemu Hans Poppe katika safari yake ya mwisho duniani.

Mbali na dalali viongozi mbalimbali wakiwemo Rais wa TFF Wallace Karia, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Almas Kasongo, wamejumuika kumsindikiza.

Wakati wa uhai wa Hans Poppe alikuwa akiisaidia Simba katika usajili akiwa Mwenyekiti kamati ya usajili Kamati ilivyokuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha mchezaji waliyemuhitaji  anapatikana.

Baada ya mabadiliko ya uendeshaji katika Klabu ya Simba, Hans Poppe alikua ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.