Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 25Article 574078

Soccer News of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mastaa waishitaki Azam FC

Aggrey Morris miongoni mwa nyota waliosimamishwa Aggrey Morris miongoni mwa nyota waliosimamishwa

Baada ya wiki kadhaa zilizopita klabu ya Azam FC ya Jijini Dar es Salaam kutoa taarifa juu ya kuwasimamisha wachezaji wake watatu, Agrey Moris, Salum Abubakar na Mudathir Yahya kwa muda usiojulikana kwa kile ilichodai ni utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao wamepeleka malalamiko yao katika Chama cha wachezaji nchini ili angalau wapatiwe ufumbuzi katika kile ambacho wanaona wao kuwa sio sawa kwa kupande wao na kanuni pia zimekiukwa katika suala hilo.

Akithibitisha hilo ,Mwenyekiti wa Chama cha wachezaji wa Soka Tanzania, Musaa Kisoki amesema;

"Wachezaji wamekuja kulalamika kuwa wamesimamishwa kuwa wachezaji wa Azam kwa muda usiojulikanan na sisi tukafanya uchunguzi na tumegundua Azam wamevunja kanuni za kuwafungia wachezaji kutoka kwenye kanuni za klabu za adhabu za klabu kwa wachezaji"

"Kwa hiyo tukaandika barua kwa Shirkikisho la Mpira nchini kwa maana kamati ya Katiba, Sheria na hadhi za wachezaji ili waweze kulifanyia kazi suala hili na hivi sasa tunasubiri kikao cha kamati hiyo" amesema Kisoki

Kwa kawaida vilabu vinaruhusiwa kumpa adhbu mchzaji lakini sio kiholela au kwa kukomoa kuna taratibu maalum (kikanuni).

Kuna mambo ambayo klabu inapaswa kufuata pindi wanapotaka kumpa adhabu mchezaji sio tu unatamka muda usiojulikana , katika utoaji wa adhabu kikanuni hakuna kitu kama hicho.