Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 10Article 562354

Soccer News of Sunday, 10 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Matokeo Championship, DTB yakwama

Matokeo mechi za Championship Matokeo mechi za Championship

Ligi ya Championship jana Oktoba 9 imeengia katika hatua ya raundi ya pili ambapo viwanja mbali mbali viliwaka moto.

Vinara wa Ligi timu ya DTB, ilishuhudia ikivutwa shati na kulazimishwa sare ya magoli 1-1 na timu ya Green Warriors huku wakishuhudia mshambuliaji wake Amisi Tambwe alishindwa kumaliza mchezo baada ya kufanyiwa madhambi.

Hali kadhalika timu ya African Sports imetoa kipigo kizito cha magoli 4-0 dhidi ya Mwadui FC.