Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 12Article 562837

Soccer News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Morrison aandaliwa Ulinzi mzito Botswana

Winga wa klabu ya Simba,Benard Morisson Winga wa klabu ya Simba,Benard Morisson

Wapinzani wa Simba katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika Jwaneng Galaxy kutoka Botswana ni kama wameAnza kuingiwa na mchecheto baada ya kocha wao mkuu Morena Ramoreboli kumtaja winga wa Simba Bernard Morrison kama mmoja wa wachezaji hatari wa timu hiyo na anatakiwa kuchungwa sana.

Jwaneng Galaxy wakiwa nyumbani kwao nchini Botswana wanatarajiwa kucheza na Simba katika wa kwanza wa raundi ya kwanza ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo katika mchezo utakaofanyika Octoba 17, katika uwanja wa timu ya taifa ya Botswana.

Kocha Morena alisema kuwa kikosi cha Simba kimesheheni wachezaji wazuri huku akimtaja winga Bernard Morrison kuwa ndiye mchezaji tishio ambaye aliwahi kumshudia wakati akiwa anakipiga katika klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini jambo ambalo anaamini wachezaji wake wanatakiwa kuwa makini na winga huyo.

“Licha ya ubora wa Simba kama timu lakini ina wachezaji wengi wazuri mmoja namfahamu vyema ni Bernard Morrison kwa kuwa nilimshuhudia akiwa katika klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

“Ni mchezaji mzuri na mwenye kasi ambaye anahitaji ulinzi mzuri ili asilete madhara, kwa upande wetu tunafahamu kuwa tunaenda kucheza na timu bora hivyo tutahitaji kuonyesha ubora wetu dhidi yao ili tushinde mchezo tukiwa nyumbani,”alisema kocha huyo.