Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 23Article 573664

Soccer News of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mourinho amzawadia viatu dogo aliyempa matokeo (+Video)

Mourinho ampa zawadi ya Viatu Felix Afena-Gyan Mourinho ampa zawadi ya Viatu Felix Afena-Gyan

Juzi Jumapili Mourinho na As Roma, walikua ugenini katika mchezo mgumu dhidi ya Genoa na mpaka wanakwenda mapumziko bado walikua sare ya 0-0.

Kipindi cha pili dakika ya 74, Mourinho alimuinua kinda Felix Afena-Gyan kutoka benchi na kumuingiza kitendo kilichowashangaza wengi.

Felix Afena-Gyan hakumuangusha Mourinho kwani alifunga mabao mawili dakika za 82' na 90 + 4', na kuandika rekodi katika Ligi ya Serie A, ya kuwa mchezaji mdogo kufunga ndani ya Ligi hiyo.

Afena-Gyan amezaliwa mwaka 2003. Kitendo hicho kilimfurahisha Mourinho na kuahidi kumnunulia zawadi ya viatu vya ndoto yake kinda huyo.

Sasa Mourinho ametimiza ahadi yake kwa kumkabidha Afena-Gyan zawadi ya viatu vyenye thamani ya Euro 800 sawa na shilingi za kitanzania 2073800.

Tazama Video hapa chini;