Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 06 03Article 540766

Soccer News of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Mpango wa KMC wakiendelea kuwawinda Dodoma Jiji

Mpango wa KMC wakiendelea kuwawinda Dodoma Jiji Mpango wa KMC wakiendelea kuwawinda Dodoma Jiji

Kikosi  cha KMC kimeendelea kujifua kuelekea katika michezo ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu 2020/2021 ambapo itakuwa ugenini Juni 17, 2021 kukipiga na Dodoma Jiji  katika Uwanja wa Jamuhuri Jijini Dodoma.

Submitted by George David on Alhamisi , 3rd Jun , 2021 Kocha msaidizi wa KMC, Habib Kondo na Kocha mkuu wa klabu hiyo, John Simkoko wakiteta jambo wakati kikosi cha KMC kikiendelea kujifua kuwawinda Dodoma Jiji Juni 17.

Mipango ya makocha, Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Habibu Kondo ni kuhakikisha kwamba KMC inafanya vizuri na hivyo kuendelea kusonga mbele katika michezo mingine iliyosalia.

Simkoko amesema, “Tunaendelea na maandalizi, wachezaji wote wanamorali na hari ya kuhakikisha kwamba kile ambacho wanaelekezwa na makocha wanakifanyia kazi kwenye michezo husika jambo ambalo linawezekana kwakuwa michezo yote licha ya kwamba itakuwa na ushindani mkubwa lakini bado ipo ndani ya uwezo wa KMC FC".

Aidha Kino Boys hivi sasa imebakiza michezo mitano ambayo kati ya hiyo minne itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru Jijini Dar es Salaam huku mmoja ambao ni dhidi ya Dodoma Jiji utakuwa ugenini ambapo Timu na uongozi kwa ujumla inaendelea kujipanga ili kuhakikisha kwamba inafanya vizuri na hivyo kumaliza msimu ikiwa kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa Ligi kuu.

Michezo ambayo KMC FC imebakiza kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2020/2021 hivi sasa ni dhidi ya Dodoma jiji, Mtibwa Sugar, JKT Tanzania ,Simba pamoja na Ihefu huku ikiwa imeshacheza michezo 29 na kujikusanyia alama 41 na kuwa kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa Ligi Kuu.

 

Join our Newsletter