Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 14Article 563125

Soccer News of Thursday, 14 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

"Ni kufa au kupona Jumapili" -Bocco

Nahodha wa Simba, John Bocco Nahodha wa Simba, John Bocco

Nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco, amesema wamejipanga vema kuhakikisha wanaanza vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itapambana na timu ya Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumapili hii huo ukiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza.

Akizungumza mara baada ya mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mo Arena Bunju, Bocco amesema kinachowapa shauku ya kushinda ugenini ni maandalizi mazuri pamoja na ubora wakikosi walichonacho so much huu.

"Maandalizi yetu yanaendelea vizuri wachezaji tunahamasa kubwa na lengo letu ni kushinda mechi zote mbili ili kutinga hatua ya makundi kama ilivyokuwa msimu uliopita," amesema Bocco.

Taarifa njema kwa mashabiki wa timu hiyo ni kwamba wachezaji wote waliokuwa majeruhi tayari wamepona na walishaanza mazoezi wakiwemo Shomary Kapombe, Papy Sakho na Sadio Kanoute.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini kesho Alhamisi kuelekea Botswana tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumapili saa 10 jioni kwa saa za Tanzania.