Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585901

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Nyota Bayern akumbwa na matatizo ya moyo

Beki wa Bayern Munich, Alphonso Davies Beki wa Bayern Munich, Alphonso Davies

Kocha wa klabu ya Bayern Munich Nagelsmann amethibitisha kumuacha Alphonso Davies kutokana na matatizo ya moyo yaliogundulika baada ya kufanyiwa vipimo hivi karibuni.

Alphonso Davies amekosa mchezo wake wa kwanza mwaka 2022 ambao Bayern walishindi 2-1 dhidi ya Gladbach baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19, lakini kwa sasa amepima na kukutwa hana maambukizi na alitarajiwa kurudi mazoezi baada ya madaktari wa timu kuthibitisha.

Kwa bahati mbaya kwenye vipimo kitu kisicho cha kawaida kikagundulika kwenye moyo na sasa atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiendelea na matibabu ya moyo.

“Jana wakati tunafanya vipimo ambavyo tunafanya kwa kila mchezaji kujua kuwa ana maambukizi ya uviko-19, katikati ya kipimo tuligundua ishara isiyo ya kawaida kwenye moyo wa Davies, ila kwa sasa amesimama mazoezi, na hatakuwepo kwa wiki kadhaa zijazo.” Alisema Nagelsmann.