Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 12Article 562774

Soccer News of Tuesday, 12 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Nyota Twiga Stars, afunguka ugumu wa mashindano, amsifu Kocha

Mchezaji wa Twiga Stars, Fatuma Issa play videoMchezaji wa Twiga Stars, Fatuma Issa

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake "Twiga Stars", Fatuma Issa, "Fetty Densa" ameweka wazi kuwa mashindano ya COSAFA yalikuwa magumu lakini wanamshuku Mungu kwa kuweza kuwa nao mpaka mwisho wa siku wakafanikiwa kutwaa taji hilo.

Oktoba 11 timu ya Twiga Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Bakari Shime iliweza kurejea Tanzania na kupokewa na mashabiki pamoja na viongozi wa Serikali bada ya kurudi na taji la COSAFA ambalo wamelitwaa nchini Afrika Kusini.