Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 10 13Article 562966

Soccer News of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Nyota wa Yanga ataka kufunga mabao

Mshambuliaji wa Yanga, Yusuph Athumani Mshambuliaji wa Yanga, Yusuph Athumani

Mshambuliaji mpya wa Yanga, Yusuph Athumani amesema kuwa anahitaji kupambana kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha ili yamfanye awe anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

Yusuph Athumani ambaye amejiunga na Yanga katika dirisha kubwa lililopita la usajili anapata upinzani mkali wa kuanza katika kikosi cha kwanza mbele ya washambuliaji wenye uraia wa DR Congo, Fiston Mayele na Heriter Makambo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Yusuph amesema kuwa anahitaji kufunga mabao ya kutosha pindi anapopata nafasi ya kucheza kwani anaamini akifanya hivyo atamshawishi kocha kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

“Hakuna njia nyingine ya mimi kuweza kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kama kufunga,malengo yangu ni hayo ni kufunga katika nafasi ambayo nipata yakucheza hiyo naamini itamshawishi mwalimu kunipatia nafasi mara kwa mara.

“Ushindani wa namba ni mkubwa lakini naamini kila mchezaji atacheza kwa wakati wake na kwa mipango ya mwalimu lakini yote ni kwaajili ya kuisadia Yanga kufanya vyema,”amesema mshambuliaji huyo.