Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 11Article 585034

Soccer News of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Oscar Kumrithi Philippe Countinho Barcelona?

Oscar Oscar

Barcelona wametajwa kuwa wamemgeukia nyota machachari wa Brazili Oscar, maarufu kama Oscar dos Santos Emboaba Junior.

Coutinho, ambaye ana miaka 29 amerejea Ligi Kuu Uingereza akisaini na Aston Villa kwa mkopo wa awali wa miezi sita, huku klabu hiyo ikiwa na kipengele cha kuchagua kumnunua kwa €40m msimu wa joto.

Taarifa zinasema kuwa kocha wa Barcelona Xavi Hernandez na raisi Joan Laporta wanatazamia kuajiri kiungo mwingine mwenye ufundi wa kuisaidia Barcelona kupiga hatua kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili wa mwezi Januari.

Ripoti zinataja kuwa klabu ya Barcelona tayari imeshafanya mawasiliano na klabu yake ya sasa ya Shanghai Port kuulizia upatikanaji wake.

Hata hivyo, kuna wasi wasi juu ya upatikanaji wa staa huyo Barcelona kwa kuzingatia hali ya klabu hiyo kiuchumi.

Oscar ambaye mkataba wake wa sasa unadumu hadi Novemba 2024, amecheza Jumla ya gemu 170 akiwa na Shanghai Port, akifunga magoli 50 na asisti 93.