Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2022 01 14Article 585925

Soccer News of Friday, 14 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

PICHA 4: Kikosi cha Yanga tayari kimewasili Tanga kuwakabili Coastal Union

Sehemu ya msafara wa Kikosi cha Yanga Sehemu ya msafara wa Kikosi cha Yanga

Kikosi cha Yanga tayari kimefika Jijini Tanga, tayari kwa maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Coastal Union Jumapili.

Yanga itakuwa wageni wa Coastal katika dimba la Mkwakwani huku wakijua fika wanahitaji alama tatu ili kutengeneza mazingira ya kunyakua ubingwa walioukosa kwa miaka minne mfululizo.

Miongoni mwa wachezaji waliomo kwenye msafara wa Kikosi hicho cha Yanga ni Ibrahim Bacca ambaye amesajiliwa siku chache zilizopita kutokea KMKM ya visiwani Zanzibar.

Tazama Picha hapa chini kuona namna kikosi hicho kilivyowasili;