Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 22Article 573589

Soccer News of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pedri ashinda Tuzo ya Golden Boy

Kinda wa Barcelona, Pedri Kinda wa Barcelona, Pedri

Kiungo wa Barcelona Pedri ametajwa kuwa mshindi wa tuzo ya Golden Boy mwaka 2021 na kumbwaga Jude Bellingham wa Borussia Dortmund, Pedri mwenye umri wa miaka 18 anakuwa mchezaji wa pili wa Barca kushinda tuzo hiyo tangu aliposhinda Lionel Messi mwaka 2005.

Pedri alijiunga na Barecelona akitokea klabu ya Las Palmas mwaka 2020 majira ya joto, na alikuwa mchezaji tegemezi kwa Barca na timu ya taifa ya Hispania akifanikiwa kutwaa mataji ya Cop del Rey na kuvaa medali ya silva kwenye michuano ya Olympic ya Tokyo.

Pedri anafuata nyayo za Erling Haaland,Joao Felix Matthijs de Ligt ambao wameweza kushinda kama wachezaji bora wa chini ya umri wa miaka 21 kwa misimu ya hivi karibuni.

“Nawashukuru Tuttosport kwa tuzo hii ambayo inanifanya nijivunie. Asante pia kwa washiriki wote wa jury na mashabiki ambao wamekuwa wakiniunga mkono kila wakati katika 2021 hii nzuri kwangu, “alisema.

“Na bila shaka, shukrani nyingi kwa Barca, timu ya taifa, familia yangu, marafiki zangu na bila shaka kwa wale wote ambao wamekuwa karibu nami siku baada ya siku ambao bila ya wao nisingeweza kushinda Golden Boy.”