Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 24Article 573808

Soccer News of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pengine ni nafasi ya Chelsea kutetea Ubingwa wa Ulaya

Chelsea wanafurahisha kuwatazama Soka lao kwa sasa Chelsea wanafurahisha kuwatazama Soka lao kwa sasa

Mabingwa watetezi, klabu ya Chelsea wameibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya kibibi kizee cha Turin, Juventus, katika mchezo wa Kundi H, Ligi ya Mabingwa barani Ulaya usiku wa jana katika Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.

Mabao ya The Blues yalifungwa na Trevoh Chalobah dakika ya 25, Reece James dakika ya 55, Callum Hudson-Odoi dakika ya 58 na Timo Werner dakika ya 90+4.

Sasa gumzo kwa sasa sio ushindi tu waliopata Chelsea bali ni kiwango bora ambacho wanakionesha kwa sasa katika michezo yao.

Usiku wa jana Chelsea walikua bora kila eneo la uwanja, kuanzia golikipa mpaka idara ya ushambuliaji, wakiwa na mpira na wanapopoteza mpira.

Thomas Tuchel huenda ana kila sababu ya kutamani kutetea ubingwa aliobeba msimu uliopita mbele ya Man City, na ubora walionao hivi sasa unatosha kuonesha namna wanavyoweza kupambana na vigogo kulinda taji hilo kwa mara nyingine.

Kwa ushindi huo, Chelsea inafikisha pointi 12 na kupanda kileleni ikiizidi wastani wa mabao tu Juventus baada ya wote kucheza mechi tano na zote zinafuzu hatua ya 16 Bora mbele ya Zenit yenye pointi nne na Malmo pointi moja.