Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 21Article 573271

Soccer News of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pepe kwenye mipango ya AC Milan

Winga wa Arsenal, Nicolas Pepe Winga wa Arsenal, Nicolas Pepe

Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuingia kwenye orodha ya vilabu vinazowania saini ya mshambuliaji wa Arsenal Nicolas Pepe.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amekuwa na wakati mgumu kuendana na thamani ya bei yake ya pauni milioni 72 tangu awasili miaka miwili iliyopita na amepoteza ushawishi kwa Mikel Arteta.

Pepe anatajwa kuwa atamaliza kibarua chake na Arsenal mwaka 2022, huku The Gunners wakidaiwa kuwa tayari kupunguza hasara na kumuuza kwa kwa kitita cha pauni milioni 25.

Crystal Palace wanadaiwa kuweka mipango ya kuingia windoni kumnunua Pepe, lakini Il Milanista wanaripoti kwamba Milan wanatumai kuingia moja kwa moja kwenye dili na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa bosi wa Rossoneri Stefano Pioli ni shabiki mkubwa wa mchezaji huyo wa zamani wa Lille, na wenye uwezo wa kuwa Arsenal hawajaridhishwa na mchango wa Pepe.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kuweka nyavuni mabao 25 na asisti 18 katika mechi 98 alizoichezea The Gunners lakini ameanza kwenye mechi moja tu kati ya sita za mwisho za Ligi Kuu ya Uingereza.