Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 11 24Article 573916

Soccer News of Wednesday, 24 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Pitso amkingia kifua Miquissone, Waarabu wakimtengenezea Zengwe

Luis Miquissone akioneshwa maeneo ya Klabu ya Al Ahly Luis Miquissone akioneshwa maeneo ya Klabu ya Al Ahly

Licha ya kuwa hata msimu mmoja hajamaliza, tayari maswali yameanza kuibuka kutoka kwa mashabiki, waandishi na baadhi ya nguli wa Klabu ya Al Ahly ya Misri juu ya kiwango cha mchezaji Luis Miquissone ambaye alisajiliwa akitokea Simba mwanzoni mwa msimu huu.

Kumekuwa na imani kuwa ubora ambao waliutegemea wakati wanamsajili ni tofauti na kile kinachoonyeshwa na mchezaji huyo uwanjani.

Pamoja na maneno hayo juu ya winga huyo, Kocha wa Al Ahly, Pitso Mosimane amemkingia kifua nyota huyo aliyesumbua Tanzania kwa kiwango bora. Wikiendi hii katika mkutano na wanahabari baada ya mchezo Al Ahly kushinda mabao 3-2 dhidi ya Al Ghazl, Pitso alishindwa kujizuia na kujibu kwa hasira alipoulizwa swali na mwandishi wa habari kuhusu kiwango cha Luis.

Mwandishi alitaka kujua kwa nini hamchezeshi kijana mdogo (mzawa) ambaye ana kiwango bora zaidi kuliko Luis, swali ambalo wazi lilionekana kumkera na kujibu:

"Kwa hiyo unataka Luis akae benchi? Kwa nini, mbona wachezaji wengine hujauliza, kwa nini Luis?

"Luis ni mchezaji wa Al Ahly na atacheza hapa, atapata nafasi kama Hamdy na atapata nafasi kama wachezaji wengine, kila mmoja ni mchezaji wa Al Ahly, hapa atacheza.

"Nitamtoa Tau, nitamtoa Sherif na nitamtoa hata Afsha, hapa hakuna staa, wachezaji wote ni sawa."