Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556534

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Polisi Tanzania kuwapigisha gwaride Ligi Kuu 2021/2022

Kikosi cha Polisi Tanzania Kikosi cha Polisi Tanzania

Kikosi Cha maafande wa Polisi Tanzania kimeweka kambi yake kule Jijini Mwana na kikiendelea kujifua kwa ajili ya kuwapigisha kwata wapinzani wao katika mechi za Ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Polisi Tanzania wamejifua kwa takribani masaa yasiyopungua matatu kuanzia saa 1 mpaka saa 4 asubuhi.

Ikiwa Jijini Mwanza Timu ya Polisi inafanya mazoezi yake kwa awamu mbili yaani Asubuhi na Jioni ambapo asubuhi hufanyia nyamagana na ikifika jioni huamia Uwanja wa CCM Kirumba.

Kocha Mkuu Malale Hamsini na Msaidizi wake George Mketo wanaelekeza wachezaji wachezaji usahihi wa kupiga pasi, ufungaji mabao, kutumia vyema nafasi za mabao na kuimarisha ulinzi katika safu ya ulinzi huku Kocha huyo akirejea baadhi ya mabao ya uzembe waliyofungwa msimu uliopita kutokana na mabeki kutotimiza majukumu yao.

Akizungumzaa na wachezaji wake wakati akihitimisha mazoezi hayo, Malale amewachimba mkwara akiwatishia kuwa watafunga virago warudi Moshi kupumzika kama hawatosikiliza na kuyatimiza kwa usahihi maelezo yanayotolewa.

Wakati akichimba mkwara huo wachezaji walisikika wakimsihi asifanye hivyo wakisisitiza watajitahidi kuonyesha uwezo wao ili malengo ya kambi yatimie.

"Hivi kwanini wewe Datius (Peter) kwanini unakaa na mpira muda wote huo unatafuta nini, chukua mpira toa kwa mwingine twende mbele. Kama ndiyo hivi tutapaki mabegi tukapumzike tu si ndivyo mnavyotaka," amesikika akisema Malale.

Beki mpya wa timu hiyo, Juma Makapu ameiambia amesema kuwa maandalizi ya kikosi Chao yanakwenda vizuri kutokana na jitihada za benchi la ufundi kuhakikisha wanatengeneza timu nzuri ya kushindana huku wachezaji nao wakijitahidi kufuata maelekezo hayo.

"Maandalizi yanakwenda vizuri na kikosi chetu ni kizuri wachezaji tunajitahidi kuhakikisha tunayafanyia kazi maelekezo ya walimu wetu, bila shaka tutafanya vizuri," amesema.

Aidha wachezaji wengi wa Polisi wamepanga kutoa upinzani wa kutosha msimu wa Ligi utakapoanza kwa kujinasibu kuwa wako vizuri kupita maelezo.