Uko hapa: NyumbaniMichezoMpira wa Miguu2021 09 10Article 556741

Soccer News of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Price Dube nje wiki sita

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube

Mshambuliaji hatari wa Azam FC, Prince Dube atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita kutokana na upasuaji mdogo aliofanyiwa baada ya kupata majeraha.

Tangu msimu uliopita Dube hakua na mwendelezo mzuri baada ya kupata majeraha ya mara kwa mara na kukosa baadhi ya michezo ya ligi kuu na ile ya Kombe la Shirikisho mfano dhidi ya Simba katika mchezo wa nusu fainali.

Akithibitisha hilo Ofisa habari wa Azam FC Thabit zakaria "zaka zakazi" amesema

"Unajua tatizo la majeraha ya Dube ni la muda kidogo, naweza kusema tangu msimu uliopita ila limekua la kujirudia rudia kila wakati"

"Sasa wataalamu waliokuwa wakimuhudumia wameona wamfanyie upasuaji mdogo ambao utamweka nje kwa wiki zipatazo sita, kwa sasa Dube yupo Afrika ya Kusini katika mji wa Cape Town na anaendelea vyema kabisa" amesema zaka zakazi

Azam leo hii Septemba 10 inashuka Dimbani huku ikimkosa mfumania nyavu huyo, katika mchezo wa awali wa kombe la Shirikisho Afrika dhidiya timu ya Horseed kutoka nchini Somalia na Mchezo huo hautahudhuriwa na Mashabiki.